Eckros Driving School

Eckros Driving School Ni chuo bora cha udereva nyanda za juu kusini

*MFUMO WA _P*S_ NI STENDI KIGANJANI MWAKO*Ndugu Abiria,Umewahi kusikia kuhusu mfumo wa P*S? Basi k**a hujawahi kusikia, ...
06/10/2024

*MFUMO WA _P*S_ NI STENDI KIGANJANI MWAKO*

Ndugu Abiria,
Umewahi kusikia kuhusu mfumo wa P*S? Basi k**a hujawahi kusikia, fahamu kuwa LATRA sasa wamekuletea stendi kiganjani mwako. Kwa kutumia mfumo wa P*S, unaopatikana katika kiungo (link) cha https://pis.latra.go.tz/, sasa hivi unaweza kujua na kufanya yafuatayo:
1. *Kujua muda ambao basi litawasili katika kituo unachotaka kuanzia safari au kulisubiria*;
2. *Kujua muda unaotarajia kufika kule uendako*;
3. *Kujua mwendokasi wa gari unalosafiri nalo au jingine lolote lililopo barabarani*
4. *Kujua jina la mmiliki wa gari husika litakalowasili kwenye kituo ulichopo*
5. *Kujua kituo cha mwisho gari lililokuwepo au lilipo kwa muda huo kabla ya kufika ulipo au kule linakoelekea*
Taarifa hizo pia zitakuwa zinapatikana kupitia skrini (screens) zilizopo kwenye vituo vyote vikuu vya mabasi. Baada ya kupata taarifa unayohitaji sasa ni rahisi kwako kuingia kwenye mfumo wa basi husika na kukata tiketi, ikiwa shida yako ilikuwa kusafiri au kuendelea kumsubiria mgeni wako, au kujiridhisha tu.
Ni rahisi sana kutumia. Chukua simu yako ya kiganjani ingia kwenye Google au Mozilla firefox, andika https://pis.latra.go.tz/ au P*S LATRA kisha, tafuta (search), mfumo utafunguka na kukuleta ukurasa wa kwanza utakaokuwa na sehemu mbili: Vituo vya Mabasi (Bus Stations) na Mwendokasi wa Basi (Bus Speed). K**a unataka kujua ratiba ya kuwasili kwa basi husika basi bonyeza Vituo vya Mabasi kisha huko ndani utachagua kituo husika. K**a unataka kujua mwendo wa basi unalosafiria basi bonyeza mwendokasi wa basi. Hapo utaingiza namba ya basi husika kisha itakuletea taarifa nzima ya mwendokasi wa basi hilo kwa siku ulizochagua.
Kutokana na ukweli kuwa sasa unaweza kujua basi fulani liko wapi au litawasili muda gani, na kutokana na ukweli kuwa unaweza kukata tiketi mtandaoni kwa kutumia link ya mtandao wa basi husika, kazi ya stendi za mabasi imeanza kupungua siku hadi siku. Kazi pekee iliyobaki ni kuwa kituo cha kusubiria gari tu au kushukia.

IWUNGILO ASANTENI KITUO KINACHOGUATA  TUTAKIWEKA HAPA. Usalama barabarani ni jukumu letu sote
28/08/2024

IWUNGILO ASANTENI KITUO KINACHOGUATA TUTAKIWEKA HAPA. Usalama barabarani ni jukumu letu sote

CHAMA CHA SHULE BINAFSI ZA UDEREVA TANZANIA TUKIWA DODOMA
30/07/2024

CHAMA CHA SHULE BINAFSI ZA UDEREVA TANZANIA TUKIWA DODOMA

*RIPOTI MPYA YA HALI YA USALAMA BARABARANI DUNIANI (GLOBAL STATUS REPORT 2023) IMETOKA TAREHE 13/12/2023*Kwa mujibu wa R...
14/12/2023

*RIPOTI MPYA YA HALI YA USALAMA BARABARANI DUNIANI (GLOBAL STATUS REPORT 2023) IMETOKA TAREHE 13/12/2023*

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, ajali za barabarani bado ni janga kubwa linaloisumbua dunia. Juhudi mbalimbali zilizochukuliwa tangu kutolewa kwa ripoti ya mwanzo zimeonesha mafanikio kwa kiasi chake, japo juhudi bado zinahitajika. Kwa hali ilivyo sasa:-
1. Watu 1.19 Milioni wanafariki kwa ajali za barabarani duniani, ambayo ni sawa na vifo 15 katika kila watu 100,000. Hii ni sawa na upungufu wa vifo wa 5% tangu 2010.
2. Ajali za barabarani bado zimeendelea kua chanzo nambari moja cha vifo vya watoto na vijana kati ya umri wa miaka 5 hadi 29
3. Ajali za barabarani ni chanzo nambari 12 cha vifo vyote ulimwenguni
4. Abiria wa Magari wanaunda 30% ya vifo vyote ulimwenguni
5. Waenda kwa miguu wanaunda 23% ya vifo vyote ulimwenguni
6. Boda boda na Bajaji wanaunda 21% ya vifo vyote ulimwenguni
7. Wapanda basikeli wanaunda 6% ya vifo vyote ulimwenguni
8. 92% ya vifo vyote vinavyotokana na ajali vinatokea katika nchi zenye uchumi wa chini na wa kati (LMICs)
9. Uwezekano wa kifo ni mara 3 zaidi katika nchi masikini na zenye uchumi wa kati kuliko katika nchi zilizoendelea.

Unaweza kupakua ripoti hiyo hapa: https://www.who.int/teams/social-determinants-of-health/safety-and-mobility/global-status-report-on-road-safety-2023?mc_cid=66d30a4bf2&mc_eid=5c3893cda0.

Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote

Hongera wahitimu, Tanzania bila ajali inawezekana
17/10/2023

Hongera wahitimu, Tanzania bila ajali inawezekana

ALAMA HII IPO KATIKA KUNDI GANI?
01/09/2023

ALAMA HII IPO KATIKA KUNDI GANI?

Karibu sana Eckros driving school, usalama barabarani ni jukumu letu sote0762795251
30/05/2023

Karibu sana Eckros driving school, usalama barabarani ni jukumu letu sote
0762795251

30/05/2023

Ndugu zangu ambao muna leseni na hamuna vyeti vya mafunzo ya udereva karibuni sana Eckros driving school
Tupigie 0762795251

Nini utofauti wa alama hizi mbili?
30/05/2023

Nini utofauti wa alama hizi mbili?

Dereva bora anaandaliwa hapa
01/02/2023

Dereva bora anaandaliwa hapa

01/02/2023

Mafunzo ya udereva yanaendelea

Address

Njombe

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Eckros Driving School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Eckros Driving School:

Share