BabaAfricatz

BabaAfricatz machenics technician Sales and buy

19/11/2025
 . Kwenye injini za diesel ndani ya silinda maeneo ya juu, kwenye piston crown au kwenye silinda head maeneo maalumu huw...
03/07/2023

.

Kwenye injini za diesel ndani ya silinda maeneo ya juu, kwenye piston crown au kwenye silinda head maeneo maalumu huwa kunakuwepo na kichumba maalumu kwaajili ya kuwezesha muunguzo kufanyika.
Chumba hicho kitaalamu huwa kinaitwa COMBUSTION CHAMBER yaani chumba cha mwako. Miundo ya chumba cha mwako pamoja na ukubwa huwa unatofautiana, hii ni kwa sababu miundo ya injini huwa inatofautiana na kwamba namna ya uchomaji pia huwa inatofautiana.

.
•Direct combustion chamber
•Indirect combustion chamber.

1.DIRECT COMBUSTION CHAMBER katika muundo huu wa chumba cha mwako huwa kinajengwa juu kwenye piston crown, piston kwa juu huwa panawekwa shimo kwa mfumo maalumu na kwamba, katika muundo huu nozeli huwa inatema diesel moja kwa moja kwenye chumba cha mwako.
✓(Angalia picha ya kushoto).
Kutokana na muundo huu wa chumba cha mwako jinsi kilivyo, wakati wa mgandamizo(compression stroke) kiwango cha joto kinachopotea ni kidogo, kwa maana hii mfumo wa upashaji joto sio lazima sana, ingawa injini zingine za direct injection k**a ilivyo kwa Tdi300 huwa wanaweka, imefanywa hivyo kwa madhumuni ya kuisaidia injini kuwaka kwa urahisi wakati injini inapokuwa na kiwango kidogo cha mgandamizo na kwenye mazingira ya baridi sana, vinginevyo injini ambazo ni direct injection zinaweza kuwaka bila ya kutegemea mfumo wa heater.
.
•saurer turbulence
•swirl turbulence
Miundo hii huwa inatofautiana hasa kwa namna ambavyo hewa inaingia na kuzunguka kwenye chumba cha mwako, saurer turbulence ni chumba cha mwako ambacho kimetumika sana kwenye injini nyingi zinazotumika kwenye magari makubwa(automotive diesel engines).


√ Uwiano wa mgandamizo katika muundo huu ni mdogo k**a vile 13:1 mpaka 16:1 wakati indirect injection huitaji uwiano wa mgandamizo wa 16:1 hadi 23:1.

√mfumo wa upashaji joto sio muhimu sana,ingawa kwa sababu maalumu ,mfumo wa upashaji joto unaweza kufungwa.

√ kiwango kidogo cha ulaji mafuta.

√Hufaa sana kwa injini kubwa.


•Injini huwa inatoa makelele mengi wakati inafanya kazi.

•Inahitaji injection pump yenye presha kubwa.

•Haifai sana kwenye injini ndogo ziendazo kasi labda kwa kufanyia marekebisho maalum.

2.INDIRECT COMBUSTION CHAMBER .
K**a inavyoonekana kwenye picha ya upande wa kulia, mfumo huu wa chumba cha mwako huwa kinajengwa kwenye silinda head na kwamba kunawekwa njia maalumu kutoka kwenye silinda maeneo ya juu kwenda kwenye chumba cha mwako kwenye silinda head.
Katika muundo huu, nozeli inatema kwenye kichumba kilichopo kwenye silinda head, wakati wa mgandamizo piston inaisukuma hewa iliyogandamizwa hadi kwenye chumba cha mwako na huko injector(nozeli) inatema mafuta na kusababisha muunguzo . (kwa uelewa zaidi angalia picha).
Kitaalamu inaweza kusemwa kwamba, indirect injection inakuwa na vyumba viwili vya mwako, kimoja kinakuwepo juu kwenye piston crown kwa muundo maalumu na kingine kwenye silinda head eneo maalumu na njia maalumu ya kupitisha hewa iliyogandamizwa kutoka kwenye piston crown kwenda kwenye chumba cha mwako huwa inawekwa njia hiyo inaitwa AIR PASSAGE.

muundo huu unaweza kuitwa air cell, pre_combustion chamber au separate type.

Kutokana na jinsi muundo huu wa chumba cha mwako kilivyo, kiwango cha joto kinachozaliwa ni kidogo kwa maana hiyo, ili kuiwezesha injini kuwaka kwa urahisi katika hali ya ubaridi, ni lazima kuufunga mfumo wa upashaji joto, injini nyingi ndogo zinazotumia diesel ambazo zinakwenda kasi huwa zinatumia muundo huu wa chumba cha mwako.
.
√kelele ni kidogo wakati injini inapokuwa inafanya kazi.

√inafaa kwa injini ndogo ndogo ziendazo kasi.

√hufanya kazi kwa ulaini(smooth operation).


•Hutumia mafuta mengi kuliko ilivyo kwa direct injection.

•Inahitaji mfumo mzuri wa upoozaji wa silinda head.

•Ni lazima kutumia mfumo wa upashaji joto.

Habari niko hapa leo naomba  kusikia maswali yenu leo au mapendekezo juu ya nini mnapenda tuchapishe kwenye ukurasa wetu...
22/05/2023

Habari niko hapa leo naomba kusikia maswali yenu leo au mapendekezo juu ya nini mnapenda tuchapishe kwenye ukurasa wetu, kwani nimedhamiria kurudi kwa kishindo, baada ya muda mrefu kukaa kimya, jumbe zenu zimenipa msukumo wa kurudi tena.

Machenical technician jobs
16/06/2022

Machenical technician jobs

15/06/2022

Periodic maintenance

06/10/2021

Check hydrolic system

Address

Sabasaba
Mtwara

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00

Telephone

+255688515165

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BabaAfricatz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to BabaAfricatz:

Share