13/05/2019
JE UPO KUNDI GANI KIUCHUMI KATI YA HAYA?
Soma hapa ujifunze zaidi..
Kuna makundi manne (4) ya watu wanaotengeneza pesa hapa duniani. Na unaposoma makala hii tambua kuwa hii ni elimu inayoweza kuwa kinyume na mawazo yako and that's okay. So tuyaangalie haya makundi vizuri.
1. WAAJIRIWA.
Hawa ni watu ambao kimsingi wanauza muda wao almost wote wa siku nzima kwa mwajiri wao na yeye anawalipa pesa kwa kuwaambia cha kumfanyia. Kwa kuwa kanuni ya mshahara huwa ni kumlipa mtu angalau 10% ya anachozalisha hasa kwa makampuni makubwa basi haitakaa itokee mwajiriwa kulingana kipato na mwajiri wake. Never!
2. WALIOJIAJIRI
Hawa hujitambua kidogo na kuamua kufanya kazi binafsi au kufungua biashara ndogo k**a duka nk. Lakini kwa kuwa hawana pesa ya kununua muda wa watu wengine na kuwaajiri hawa nao huwa busy kutwa kucha bila mafanikio ya maana sana. Ana duka miaka 15 sasa halijawahi kupanuka likawa supermarket. Lakini kwa kuwa anaishi katikati ya watu masikini au fukara kabisa basi yeye huona amepiga hatua kubwa. Na mara nyingi huyu mtu akifa na biashara yake nayo humfuata. Coz kila kitu kinamtegemea yeye.
3. WAMILIKI WA BIASHARA KUBWA
Hili ni kundi la tatu. Hawa huwa na kipato endelevu maana amenunua muda wa watu weeengi kawaajiri halafu kawapa majukumu kwa hiyo awepo asiwepo pesa inaendelea kuingia kwake. Mfano kina Bakhressa. Hivi sasa unaposoma hii makala hujui Bakhressa alipo. So awepo nchini asiwepo kipato chake kinaendelea kuingia kila dakika.
4. WAWEKEZAJI
Hili ni kundi la nne.
Hawa ni watu wenye pesa nyingi zaidi na wana uwezo wa kuwekeza mahali hata nje ya nchi ikawa inawazalishia pesa zaidi bila wao kuwepo kabisa.
Kwa hiyo nadhani tayari wewe unajua kundi lipi upo katika hayo.
SASA SIKIA...
Makundi mawili ya kwanza ni makundi ya watu . Again unaposoma weka hisia zako pembeni kwanza utaelewa vizuri. Okay tuendelee.
Mfano waajiriwa ni watu wanaotumia muda wao na nguvu na maarifa yao yote (waliyoyakusanya kwa miaka mingi ya kusoma kwa shidashida lea wengi) "kumtajirisha" mtu kwa malipo kidogo yanayomwezesha huyu muajiriwa kulipa kodi (siyo kujenga), kula, kuvaa, kusafiri kwenda na kurudi kazini nk. Yaani basic needs tu. Na k**a anafanya kazi masaa 9 kwa siku. Yaani saa mbili asubuhi hadi saa 11 jioni basi anadhani kuwa anatumia masaa 9 tu kweli. Kumbe ukweli ni kuwa mtu huyo anaamka saa 11 alfajiri ina maana tuseme saa 12 asubuhi hadi saa mbili ni muda wa kuamka kuoga, kupita facebook na instagram nk na kwenda kazini. Ni masaa matatu hayo. Jioni pia saa 11 jioni akitoka kazini hadi kufika kwake ni masaa matatu mengine. So kiuhalisia hatumii masaa 9 bali 15 kwa ajili ya ajira yake. Anabaki na masaa 9 tu katika 24. Watamshauri kulala masaa 8 kiafya eti. Si ni kweli? Lakini huyu mtu hawezi kulala masaa 8 wakati anatakiwa kula, kuoga, kusali (k**a anafanya hivyo), kuongea na watu nyumbani, nk. Analala masaa manne matano. hatengi muda wa mazoezi nk Fast Forward kwa nini mtu huyu akistaafu anaweza kufa mapema mno! Maana mwili umeshachoka mno na pesa ya pension kwa mwezi ni k**a robo tu ya pesa aliyokuwa akiipata kwa mwezi alipokuwa kazini. Tuachane na hayo ya kustaafu tuangalie maisha ya ajira kidogo.
Na naomba kuwa lengo langu kuponda ajira.
Far from it!
Lengo langu ni kuleta awareness ili k**a umeajiriwa ujitathmini na k**a ukiona kuna cha kufanyia kazi katika niayosema hapa basi yafanyie kazi. Mfano nini ufanye cha ziada katika muda ambao siyo wa ajira (usiibe muda wa mwajiri) ili kufanyia kazi Plan B ya kiuchumi. Dunia ya leo pia ni ya kuwa makini sana k**a unategemea ajira tu. Angalia watu fulani waliajiriwa SHOPRITE enzi hizo. Ilipoondoka wengine wakakosa nafasi waliobaki wakaajiriwa NAKUMATT. Ikafa nayo. What next? Sasa kuna CHOPPIES.
Hapa ndo pa kuwa na Plan B mapema.
Unasikia kuhusu Benki ya fulani zinaweza kufungwa. Imagine mtu aliyeajiriwa hapo afu hana Plan B. What about you?
Tuendelee...
Na ukiangalia ndo maana maisha ya waajiriwa WENGI (siyo wote) but wengi yanafananafanana. Mfano ni wachache sana katika ajira ambao wamejenga nyumba zao binafsi kwa hela HALALI ya ajira. Bila kuchakachua. Wengi wana mikopo (which is not bad k**a haimgeuzi kuwa mtumwa wa mwajiri au wa benki). Pia k**a vile ilivyo vigumu kwa mwanafunzi kwenda chuo kwa gari lake mwenyewe alilonunua kwa pesa yake halali (wapo wachache sana) Na hivyohivyo waajiriwa kumiliki nyumba kwa mshahara.
Wengi wamepanga. Which is also not bad kwa maana ya kuwa na mahali pa kuanzia. But huo ndo uhalisia. Je utapanga milele?
........
Kundi la waliojiajiri je?
Waliojiajiri nao wako busy. K**a ana duka basi kufata mzigo yeye (hamwamini mtu), kuuza yeye, usafi yeye, kuhesabu stock yeye, ulinzi wa duka yeye ndo analinda maana analala humo humo. K**a alivyo na miguu mingi lakini spidi "kiduchu" ndivyo na huyu nae. Miguu mingi ya jongoo bila macho is equal to ZERO. Na hivyo hivyo shughuli nyingi bila maarifa is equal to ZERO. Yaani yuko busy kila saa lakini spidi ya mafanikio ni ndogo kweli kweli.
Sasa maendeleo hayaji kwa style hiyo ila kwa kuwa hajui anahisi siku moja na yeye atakuwa k**a Bakhressa. Kwani Bakhressa ndo anauza ice cream za Azam? Ndo anafungua mageti na kuendesha maroli?
KWA WANAFUNZI..
Bahati mbaya sana k**a ni mwanafunzi uko sekondari au chuo hiyo ndo ramani ya future yako. Ukimaliza chuo lazima uingie katika makundi hayo mawili ya kimaskini hasa kundi la kwanza. Shule inakuwa imeku-PROGRAM hivyo.
HATA HIVYO.. kuna njia ya kukusaidia kuweza kuhama kutoka makundi hayo mawili ya kwanza na kuingia makundi mawili ya mwisho pale juu.
Cha msingi ni Wewe kujishusha tu na kukubali kuwa unahitaji kujifunza hivi vitu. Lakini ukifikiri kuwa unajua kila kitu kuna maarifa utayakosa simply kwa kutothamini mawazo ya wengine ambao huenda ni Mungu tu anawaleta ili kukushtua kidogo upate ufahamu fulani lakini wewe aaah. Umeziba maskio na pamba umeweka. Hebu jifunze. Itakusaidia. K**a umeajiriwa na unasoma ujumbe huu hebu jiulize ajira yako ikiisha leo ghafla PAAP!! Utaanzia wapi? K**a utaandika CV tena basi kubaliana na hali halisi tu kuwa wewe hujawa na Plan B ya kuondoka katika dimbwi la umaskini. Na hapo ndo unakuta huyuhuyu analaumu serikali kwa nini yeye ni maskini. Kweli?
Usisubiri pension ndo uanze kufanya Plan B wakati ushakuwa mzee na nguvu huna tena na pengine maarifa ynayohitajika enzi hizo yanakuwa mapya mno.
Na k**a wewe ni hii ni habari njema sana maana ukaamua kujifunza vitu hivi sasa hivi na ukavifanyia kazi,then I assure you miaka miwili au mitatu mbeleni wakati wenzako option PEKEE waliyonayo ni kusambaza CV kuomba ridhaa ya kuingia kundi la kwanza la umaskini wewe utakuwa unanunua gari lako la pili au kiwanja na huenda umeanza kujenga kulingana tu na ndoto zako ni zipi. Usipoteze muda wako kudiscuss skendo za watu maarufu ilhali future yako ni skendo tosha. Be wise.
Tumieni muda mwingi kujifunza haya mambo na siyo kwenda KU-BET timu gani itashinda mechi wiki hii. Betting imekuwa ulevi mkubwa na serikali inakula kodi na wazazi hawana cha kufanya nao wako busy wanapambana na hali zao. Sasa wewe unapoteza muda na PESA kwa vitu visivyokujenga. Betting haitokujenga. Idris Sultan hajafikia hapo kwa sababu ya hela alizopata Big Brother Africa. No. Amefika hapo sababu ana TALENT na ameifanyia kazi na amefanya kazi kwa bidii mpaka leo. Usifikiri pesa nyingi za mara moja ndo zitakukwamua kimaisha. Ingekuwa hivyo walioshindaga mamilioni na BUZZ au CELTEL au VODACOM toka enzi hizo wangekuwa mamilionea wakubwa leo. Au waliowahi kushinda Big Brother wote wangeshakuwa Dewji leo. You see, pesa lazima ijengewe NJIA! Na kadri unavyoanza mapema ndo unapunguza urefu wa njia yako ya mafanikio. Maisha ni mbinu na kanuni sio kubahatisha.
Bahati mbaya ukiongea vitu vya namna hii unalipwa kwa matusi na kejeli. Ni kawaida.
Lakini naamini umeelewa nilichosema. Pesa inatakiwa ijengewe njia. Taratibu.. Siyo usiku na mchana tayari umekuwa tajiri. Acheni betting jifunzeni vitu halisi vya kujenga MFEREJI wa kipato. There's no short cut. Ukitaka kuishi maisha ya Bakhressa lazima upitie hustles alizopitia. Benito Mussolini alikuwa dictator lakini aliwahi kusema kauli moja naipenda sana: *"IF YOU WANT TO SHINE LIKE THE SUN FIRST YOU HAVE TO BURN LIKE IT"*... ukitaka kung'ara k**a jua basi kubali kwanza kuungua k**a linavyoungua!
Kuna mengi ya kushauriana. So haijalishi k**a umeajiriwa au umejiajiri au wewe ni mwanafunzi.