16/09/2026
Tarehe 12 Septemba 2026, Car & General iliungana na maafisa usafirishaji pamoja na familia zao katika maadhimisho ya HLX Day, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke.
Siku hii maalum ilikuwa ni fursa ya kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa maafisa usafirishaji katika kujenga taifa letu kupitia kazi zao za kila siku.
Mbali na kutambua juhudi zao, HLX Day 2026 iliambatana na michezo mbalimbali, burudani na shughuli za kijamii zilizolenga kuimarisha umoja, mahusiano na furaha miongoni mwa washiriki.
Car & General inaendelea kuwa bega kwa bega na maafisa usafirishaji, kuwapatia bidhaa bora, huduma zenye kuaminika na kuunga mkono shughuli zao za kila siku.