08/02/2026
Kops Ushawai Kujiuliza Ni Kwa nini Liverpool Ilimsajili Jérémy Jacquet wa Pauni Milioni 60 Badala ya Marc Guéhi wa Pauni Milioni 20? Kwa maoni yangu naona sababu zifuatazo zinaelezea suala hili;-
1. Gharama Iliyojificha: Ingawa ada ya uhamisho ya Marc Guéhi ilionekana kuwa ndogo (£20M), gharama halisi ya uendeshaji (mshahara wa £300k kwa wiki na ada za mawakala) ingeifanya klabu itumie takriban £110M.
2. Muundo wa Mishahara: Liverpool wameepuka kumpa Guéhi mshahara ambao ungemfanya kuwa mmoja wa walipwao fedha nyingi zaidi klabuni, jambo ambalo lingeweza kuvuruga utulivu wa chumba cha kubadilishia nguo.
3. Uwezo wa Baadaye (Potential): Jérémy Jacquet amechukuliwa k**a Mradi (Project) ya muda mrefu. Akiwa na miaka 20, Liverpool wanaamini wanaweza kumtengeneza kuwa Virgil van Dijk ajaye, huku wakimlipa mshahara mdogo unaokua kulingana na kiwango chake.
Na pia Jacquet ana umri mdogo kwa miaka mitano kuliko Guéhi, huku Liverpool wakimuona k**a mchezaji mwenye uwezo sawa au hata mkubwa zaidi wa maendeleo ya baadaye.
4. Sera ya FSG: Huu ni urejeo wa mfumo wa "Buy low (on wages), sell high" au kuwekeza kwenye vipaji chipukizi ambavyo thamani yake itaongezeka maradufu.
Liverpool tumefanikiwa mara nyingi kwa kuwasajili wachezaji nyota wa siku zijazo badala ya wachezaji waliokamilika tayari, jambo linalosaidia kudumisha uwiano mzuri wa mishahara, huku wachezaji wakizawadiwa mikataba bora zaidi kulingana na kiwango chao uwanjani.
Katika hali bora kabisa, Guéhi na Jacquet wote wangekuwa wachezaji wa Liverpool, lakini ni wazi kuwa kwa Guéhi, hesabu za kifedha hazikuwa tena na mantiki.