Makini Road Safety

Makini Road Safety Makini Road Safety is a non-governmental organization formed to promote road safety awareness in Tanz

In Tanzania, motor vehicles speeding have been a major factor for road accidents. We define speeding as exceeding the set speed limit and driving too fast. In our communities many people do not view adapting to speed limits and road safety guidelines as an important way to avoid crashes; in reality speeding is regarded as a factor in nearly one-third of all fatal crashes. We combine practical diff

erent methods for Road Safety awareness initiatives: educating community through our social networks, road safety video clips for drivers and pedestrians and Speed Reporting Application (MakiniApp) for passengers.

26/07/2022
Habari ya leo wadau wetu:HII NI LAZIMA!!!!!Mojawapo ya nguzo ya    ni kwamba  akiona taa ya kuangalia injini (Maarufu CH...
23/12/2020

Habari ya leo wadau wetu:

HII NI LAZIMA!!!!!

Mojawapo ya nguzo ya ni kwamba akiona taa ya kuangalia injini (Maarufu CHEKI INJINI) inaangaza/blinki hawezi kuendelea kuendesha gari. Hii ni dharura, mara nyingi inaonesha au kuashiria kuwa injini inawaka moto. Ukiendelea kuendesha, labda utasababisha uharibifu usioweza kurekebishwa, na kujisababishia gharama isiyo kuwa ya lazima.

Vinginevyo, wakati taa ya kuangalia injini inaangaza/blinki ,basi angalia aina hizi tatu za ishara ya ubovu kwenye injini:-

Kwanza:

Kasoro ya Mfumo wa Kuwasha โ€“Unaoweza husababishwa na plags mbovu /zilizokwisha, nyaya za umeme katika injini, hozi au koili

Pili

Uharibifu katika Mfumo wa Mafuta -Ikiwa ni pamoja na sindano za mafuta (injekta za mafuta), sensa ya joto au baridi.

Tatu

Uharibifu wa Injini wa ndani โ€“ Ikiwemo vichwa vya silinda (Silinda Hedi) mikanda ya muda (taiming belt), pistoni na ringi zake.



Kwa elimu zaidi kuhusu Usalama Barabarani tembelea YouTube channel yetu:

Makiniroadsafety

MAGARI YA AUTOMATICWengi wetu tukiwa katika maandalizi ya kuungana na familia zetu kwenye Sikukuu hizi mwishoni mwa mwak...
18/12/2020

MAGARI YA AUTOMATIC

Wengi wetu tukiwa katika maandalizi ya kuungana na familia zetu kwenye Sikukuu hizi mwishoni mwa mwaka kumekua na dhana kuwa ajali nyingi husababishwa na kafara zinazotolewa na watoa kafara. Lakini mtazamo na uzoefu wetu sisi tunasema si kweli bali ni kipindi ambacho kinakuwa na UVAMIZI MKUBWA wa aina za madereva feki kwa magari ya Abiria na Binafsi. Wanaposafiri mbele hukutana na tabia mbalimbali za barabara ama hali ya hewa sasa ukitaka kutumia uzoefu wako wa ulikotoka badala ya ueledi matokeo yake ni vifo kwa mfano madereva wa daladala Dar es Salaam wanasifika kwa sifa mbovu ya uendeshaji ikiwemo overtake za hovyo,kuchomekea kwa hovyo ,kuziba njia kwa hovyo sasa dereva huyu leo hii anapewa Eicher ambayo pia haijakaguliwa na mamlaka husika iliyotolewa kibali na LATRA( Zamani SUMATRA) atoe abiria Ubungo kwenda Rombo kwa kisingizio usafiri umekuwa adimu kumbe tunaweka maisha ya watu rehani na baadaye tunasingizia KAFARA.

JIANDAE kabla hujasafiri na gari yako kwenda safari ya mbali ambako hujajua tabia ya barabara na hali ya hewa ikoje unapaswa kuzingatia matumizi sahihi ya P,R,N,D,D-3,2,L,(+/- Shift).Je ni wakati gani N,D-3,2 na L zinatumika kwenye magari ya automatic?



Kwa video na elimu zaidi, Subscribe YouTube:
Makini Road Safety

KITUO CHA MAFUTA:Habari ya Jumapili mdau wetu,k**a kawaida yetu ni kujuzana vitu vidogo vidogo lakini muhimu katika matu...
13/12/2020

KITUO CHA MAFUTA:

Habari ya Jumapili mdau wetu,k**a kawaida yetu ni kujuzana vitu vidogo vidogo lakini muhimu katika matumizi ya vyombo vya moto kila siku.

Jumapili ya leo chukua hili kisha mjulishe na mwenziyo asiyejua hili kwa kumtag apate kujua ili asilete usumbufu anapokuwa KITUO cha MAFUTA.

Je ni mara ngapi umeingia kituo cha Mafuta ghafla umesahau k**a mfuniko wa tenki la Mafuta upo kushoto ama kulia na ukasababisha usumbufu kituoni hapo?

Kwa asiyejua, huo mshale kwenye geji ya Mafuta unaonesha mfuniko wa tenki ulipo (Kulia ama Kushoto),ukielekeza kulia maana yake mfuniko wa tenki upo kulia ama ukionesha kushoto maana yake mfuniko wa tenki upo Kushoto.



Kwa video na elimu zaidi, Subscribe YouTube:
Makini Road Safety

12/12/2020

Reli na Barabara

Habari mdau wa ukurasa wetu,kwa mara nyingine tunaona umuhimu wa kukumbushana machache kuhusu Usalama barabarani.

Kila ifikapo mwishoni mwa mwaka watu wengi husafiri kwenda sehemu mbalimbali kuungana na ndugu,jamaa na marafiki kwaajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Lakini wakiwa njiani kwa usafiri wa umma ama binafsi,na pengine wengine hawajawahi kuendesha gari safari ndefu ambako baadhi ya ishara ama alama zipo na alikotoka hazipo,hivyo kutokujua ama kupuuzia baadhi ya ishara na alama za barabarani,basi tumeshuhudia ama kusikia vifo vya watu wengi sehemu nyingi zitokanazo na makutano ya RELI NA BARABARA kukiwa na KIZUIZI ama LA

Hivyo chukua muda wako sikiliza video hizi mbili kwa makini, kuna jambo zuri utajifunza kisha mjulishe mwenziyo kwa kumtag hapo.


15/03/2019

MAKUTANO

Taa za kuongoza vyombo barabarani

Taa ya Njano

Taa Nyekundu

Gari

Dereva

Subscribe Youtube:
Makini Road Safety

Puma Energy demo

11/03/2019

MZUNGUKO-Part2

Kwenda moja kwa moja (njia moja)

BAJAJI

DEREVA

Subscribe Youtube:
Makini Road Safety

Britam demo

11/03/2019

MZUNGUKO

Kwenda moja kwa moja (njia moja).

BAJAJ

DEREVA

Subscribe Youtube:
Makini Road Safety

Britam demo

Ili kuungana nasi katika kutoa elimu kwa njia ya picha ama video kupitia ukurasa huu ,tunakukaribisha. ๐Ÿ“ธ  Hii imepigwa l...
09/03/2019

Ili kuungana nasi katika kutoa elimu kwa njia ya picha ama video kupitia ukurasa huu ,tunakukaribisha.



๐Ÿ“ธ
Hii imepigwa leo eneo la kilima kutoka Kikatiti kuelekea Maji ya Chai Arusha.

Katazo lililotolewa  na video zetu nne za leo.Elimu zaidi kwa njia ya video๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐ŸพSubscribe YouTube:Makini Road Safety
09/03/2019

Katazo lililotolewa na video zetu nne za leo.

Elimu zaidi kwa njia ya video๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

Subscribe YouTube:
Makini Road Safety

Address

NIC Investment House/Samora Avenue/Mirambo Street
Dar Es Salaam
78107

Opening Hours

Monday 08:30 - 16:30
Friday 08:30 - 16:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Makini Road Safety posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Makini Road Safety:

Share