FirstCar Motors

FirstCar Motors Tunawasaidia watu kununua magari JAPAN | DUBAI | SINGAPORE | UK

"Vifaa Muhimu Unavyopaswa Kuanavyo Kwenye Gari Lako"πŸ› οΈEwaaaa !!.  Sasa baada ya kununua na kumiliki ndinga Yako.  Nikaon...
21/10/2023

"Vifaa Muhimu Unavyopaswa Kuanavyo Kwenye Gari Lako"

πŸ› οΈ

Ewaaaa !!. Sasa baada ya kununua na kumiliki ndinga Yako. Nikaona si vibaya nika share na wewe mambo haya muhimu.

_Jambo_ la _:-

1. Hakikisha una JUMPER wire...
Hii ni ni kati ya kifaa Muhimu sana kuanacho , hutumika kwa ku boosting battery Yako k**a ipo down au imeisha nguvu .
..Itakusaidia kupata msaada kwa urahisi...

2. Triangle ( reflector)
Kwa wengi wetu tumezoea ni triangle πŸ˜€hii bwana unashauriwa uwenazo zaid ya Moja itakusaidia k**a umepata tatizo kwenye barabara yenye magari mengi au kwenye Kona Mtu akakuona.

Kwa wepesi Kwa sababu utakua umeweka Kila Moja kwa distance ( umbali ) wa Mita 15 -20.

3. Vile vile... unatakiwa uwe na ...fire extinguisher...

Nikifaa Muhimu kitakacho kusaidia kuzima moto pale utakapo jitokeza either kwa short ya umeme au kwa mazingira ya nje , n.k .

4. Life serving HAMMER

Hii pia ni aina ya kifaa muhimu , chenye mfano wa nyundo ila ina ka ncha kwa mbele kitakacho kusaidia k**a nikupasua kioo wakat hatar inatokea...
..Sababu hatar k**a hizo milango hua inaji lock na kupelekea Mtu kushindwa kujiokoa...

5 . Kitu Cha Tano na Cha Muhimu unatakiwa uwe na HOOK pamoja na KAMBA...
..Kwa ajili ya kukuvutia saa utakapo kua umekwama kwenye visiki au madimbwi...

6. Jambo la mwisho kwa Leo unatakiwa uwe na πŸ”¦
..Torch yenye mwanga angavu yenye water proof ili kizuia kuingiza maji nyakat za mvua...

"Ni hayo tu kwa Leo tukutane tena juma lijalo"

Tuandikie Hapo Chini, Ni Jambo Gani Unatamani Tukufungulie Kwenye Gari, na ULIFAHAMU...

KITU GANI UNACHOZINGATIA KABLA YA KUNUNUA GARI UNALATAKA ? # Kila Mtu ana ndoto ya gari lake analotaka kumiliki either l...
07/10/2023

KITU GANI UNACHOZINGATIA KABLA YA KUNUNUA GARI UNALATAKA ?

# Kila Mtu ana ndoto ya gari lake analotaka kumiliki either la ~BIASHARA au la ~SAFARI au matembezi ya hapa na pale n.k.

β€’ inapofika wakati wa kuchagua Gari wengi huangukia kwenye muonekano na kusahau ubora na uimara wa gari ulionalo.

Ndio utaenda na Mtu mwenye utaalam ila nayeye umpate mwaminifu na mwenye ufaham .

Lakini ❗Hata wewe mwenyewe unaweza kukagua na kujiridhisha na aina ya Gari unalotaka . kwa kuzingatia yafutayo :-

1. Usikague Gari wakati wa jioni au usiku au mahali pa kiza. Kusudi uweze kutambua k**a je rangi ya gari hili nalotaka kununua imerudiwa tena rangi au k**a limewahi kupata ajali n.k

2. Angalia tairi ya mbele k**a imelika upande mmoja kitaalam inaitwa ( Toe in au Toe Out ) . Basi ujue wheel alignmen, yake haipo sawa hii inapelekewa na wishborn bush zimeisha au tire roadend πŸ˜€ (lugha ya kiufundi ila tutaelewana tu ucjali)
Ukiona hivyo ujue kunashida hapoo

3. Angalia "brake fluid" pale mbele kwenye Bonet Kuna Kitank kidogo Cha Mafuta ya brake ...ukiona Mafuta taliyopo ni meusi au machafu ujue kwenye mfumo wa brake upande wa piston rubber kunashida.
β€’ au pia ukakuta Mafuta ya brake yapo chini . Ujue brake pad zako zimeisha na itasababisha piston zinazoshikilia pad kutoka na kupelekea hatar . Ikiwa unaendesha ndo kule unaskia brake zimekua ngumu , sababu ni piston ku stuck , mwisho wa siku inapelekea ajali.

Kwa Leo tuishie hapo . See you next time πŸ‘‰

Eheeeeee !!!! Wamekuja tenaaa . Kina nani hao ? ....Eee Bwana na wazungumzia " FirstCar Motors".Leo wanakuletea Gari Moj...
10/09/2023

Eheeeeee !!!! Wamekuja tenaaa .

Kina nani hao ? ....Eee Bwana na wazungumzia " FirstCar Motors".

Leo wanakuletea Gari Moja Kali ya Toyota aina ya "CROWN "πŸ‘‘

Leo nitakuelezea tu kwa ujumla kuhusiana na aina hii ya Gari . Najua umepata kuskia na kuona pia . ila Leo tuanzie hapa

Hivi unafaham Crown Ina models tofaut tofaut kulingana na matakwa ya mtu vile anavyo hitaji ?..

1. Kuna Crown Athlete hiii ni special kabisa kwa watu wa mbio mbio πŸ˜€ .

2. Crown Royal Yani jinalake tuu unaelewa .hili la kifamle , halitaki papara ,Wala kufkuzana .ukikaa ndani k**a uko paradiso vile. πŸ˜…

3.Crown Majesta aina hii pia ya crown Haina utofaut sana na Royal ila hii kidogo inafana k**a mark X hivii . Ukiiangalia Haina mambo mengi ila pia inamaajabu yake.

~~ Hayo ni machache tu k**a unafaham model ingine ya crown ....usiache kunidondoshea hapo chini kwenye comments . Eee Namna hiyo πŸ˜€

√ Kabla ya vyote tuangalie matoleo tofaut tofaut ya Gari hili CROWN.

πŸ‘ŒUnaambiwaje hili ni miongoni mwa magari yenye matoleo mengi mpaka hivi sasa limetoka toleo la 16 , mnamo mwaka 2022 na wanatazamia tena kutoa toleo lingine la 17 ifikapo mwaka 2027 .

Unaambiwa :

1 . Toleo lao la kwanza lilitoka mnamo mwaka 1955

2. Toleo la pili 1962

3.

4.

5.

6.

7.
16 .toleo la mwisho kutoa
*_2022_*

~~ Crown Bwana Ina sifa nyingi kwel ni
β€’ aina ya saloons car .

β€’ Ina mfumo wa suspension mzuri ambapo husikii mitetemo au makorogosheni huko nje .

β€’ Ina high-speed zinafaa pia kwenye mashindano .mfano ni Crown Athlete.

β€’ inakupa ku relax vizur ,viti vya nyuma na vya mbele pia ,hakuna haja ya kubana miguu . yaani inakupa uhuru .

N.k

Nik**a nimefika tamati kwa Leo ila pia ni mwanzo wa kupata taarifa nyingine nyingi mpya ya gari lako. Usiache kutufatilia tena na tena

Mnamo 1879, kijana wa miaka 16 aliacha shamba la baba yake na kuelekea Detroit.Wakati huo njia pekee ya usafiri ilikuwa ...
17/04/2023

Mnamo 1879, kijana wa miaka 16 aliacha shamba la baba yake na kuelekea Detroit.

Wakati huo njia pekee ya usafiri ilikuwa ni treni au magari ya farasi.

Na magari ya kwanza yalionekana k**a mashine za kukimbia kwa matajiri,

Mvulana huyu baadaye alimiliki kampuni ya magari ambayo ilibadilisha mwenendo wa tasnia ya magari kwa kile tunachojua leo.

Miaka 35 Baadaye baada ya kuwasili Detroit, nusu ya magari yote duniani yalikuwa yamebeba jina lake na mvulana Henry Ford aliekuwa kati ya watu matajiri zaidi katika historia ya Marekani hii ndiyo hadithi yake.

Henry Ford alizaliwa katika shamba la baba yake tarehe 30 Julai 1863 katika eneo ambalo sasa linaitwa Dearborn, Michigan,

Baba yake William Ford alikuwa na shamba ambalo kila mtu katika familia aliishi na kufanya kazi.

Akiwa mtoto mkubwa wa watoto sita, Henry alitarajiwa kuchukua nafasi hiyo.

Na kuongoza biashara ya familia, hata hivyo hakuwa k**a baba yake na alikuwa mchapakazi polepole na mkali huku Henry akijitahidi kusaidia shambani na alichukia wazo hilo.

K**a watoto wengi wa umri wake Henry hakupenda kwenda shule na hakuwahi kuvuka darasa la nane,

Alipendelea kujifunza mambo kwa muda wake mwenyewe na kutoka.

Akiwa na umri mdogo alivutiwa sana na mechanics, udadisi huu wa mashine ulimpelekea kusoma kila kipande cha mashine....

Tukutane Part Two!

Like | Comment | Share

Je ! πŸ˜€ unajua sifa na aina za Magari ya masafa marefu ?Njoo nikuonyesheπŸ‘‡πŸ‘‡Eee bwana ukiskia raha ya safari , hata Gari pi...
31/03/2023

Je ! πŸ˜€ unajua sifa na aina za Magari ya masafa marefu ?

Njoo nikuonyesheπŸ‘‡πŸ‘‡

Eee bwana ukiskia raha ya safari , hata Gari pia linahusika, je unataka kwenda wapi na unatamani kujua ni aina gani ya gari itakufaa?

Endelea kufuata nami.

β€’ Hizi ni sifa za magari ya masafa marefu, k**a lako halina sifa hizi basi ujuee 😊. Haya tuendelee :-

~ Uwezo mkubwa wa engine, hii pia ni kiashiria cha kua gari yako inauwezo wakwenda umbali au masafa marefu bila kuipumzisha.

- Uwezo huu wa engine hujulikana k**a Cc ya engine , mfano gari zenye Cc 1700,1800, 1900, 2000 nakuendelea, zina uwezo mkubwa sana kwenye safari za mbali bila ya engine kuchemsha, knock , tyre .

~ Zinauwezo wa kuhimili changamoto zote barabarani, iwe ni kwenye matope hazisubir msaada wa kuvutwa, kwenye Ardhi inayoteleza ndo zimefika , kwenye rafu (rough)road zinapita k**a zipo lami . kwann kwa sababu zimeundwa na shockup imara na zina coil zinazo himili mikiki yoote ya barabarani.

~ hua hazisumbui hata wakati wa ufanyaji wake wa service hizi bhuana ukitaka u enjoy ufunge genuine parts yaani spare original .
N.k : hizo ni miongon mwa sifa za Magari ya masafa marefu , zifuatazo ni mifano wa Magari yenye sifa za masafa marefu 😊

>Subaru Forester
>land cruiser
>Nissan patrol
>Discovery
>land rover
Na mengine mengi ambayo una cc kuanzia 1700 na kuendelea .

Najua unataman ningetaja gari lako kati ya hayo πŸ˜… ila usiache kutufatilia tena na tena , uendelee kupata updates mbali mbali.

TOYOTA  HARRIER Miongoni mwa Magari pendwa ya Toyota najua hutoacha kuzungumzia Toyota Harrier ,si ndioo ?  😊 Sawa sasa ...
07/03/2023

TOYOTA HARRIER

Miongoni mwa Magari pendwa ya Toyota najua hutoacha kuzungumzia Toyota Harrier ,si ndioo ? 😊

Sawa sasa basi Tuanzie hapaa : -

~ >Toyota Harrier ni Gari lenye mwonekano mzuri kwa nje na linavutia

~> ni Gari zenye Taa kubwa nzuri , mithili ya jicho , husaidia hata wakat Wa usiku hatakam mvua inanyesha Kuweza kuangaza vizuri .

~> ni Gari lenye uwezo Wa kubeba watu watano , haswaa k**a unafamilia ,litakufaa sana.

~> linauwezo Wa kusafiri umbali mrefu Bila kuleta athari kwenye Engine yako .

~> linaweza kuhimili changamoto zote za barabarani , hata kwenye rough road .

~> inauwezo wa kumaliza kisahani ( RPM ), kwa wale tunapenda ligi barabarani huyu mnyama ni mkalisana πŸ˜€.

β€’ Kwa Mara ya kwanza Toyota wakatoa toleo la kwanza mnamo (December 1997)

β€’ Toleo la pili mnamo mwaka ( 2003-2008)

β€’ Toleo la tatu mnamo mwaka (2008 - 2013)

β€’ Toleo la NNE mnamo mwaka (2020 - hivi Sasa)

~> kila toleo hapo juu lina model tofaut tofaut na ni nzuri . niambie umependa model gani kati ya hizo .

R~A~N~G~E R~O~V~E~R Leo ni Leo asemae kesho ni mwongoo πŸ™ƒUmewahi mskia huyu mnyama anaeitwa Range rover" . Ee bwana huyu ...
11/02/2023

R~A~N~G~E R~O~V~E~R

Leo ni Leo asemae kesho ni mwongoo πŸ™ƒ

Umewahi mskia huyu mnyama anaeitwa Range rover" .

Ee bwana huyu ni mnyama wa porini, na majini ni mnyama mkali hatari asiye na madhara.

√ Range Rover imetokana na Jina la kwanza lililofahamika k**a (Land Rover Range Rover) kushindwa kutamkika na watu wengi kutokana na urefu wa jina hilo na kuamua kulifupisha .

√ land rover ni kiwanda kilichopo united kingdom (UK) na Australia, kinacho zalisha Magari ya aina mbali mbali k**a Jaguar , Range discoveryn.k na miongoni mwa hayo range rover ni miongoni mwao .

Range rover ilifanikiwa kutoa aina tofaut tofaut za Magari kulingana na Tecknojia ilivyokua kwa wakati huo .

#1. Toleo la kwanza na kwa Mara ya kwanza kuingiza sokoni Magar yao ni mwaka (1969-1996).

# 2. Toleo la pili mwaka
(1994- 2002 )

#3. Toleo la tatu likitoka mwaka( 2002 -2012 ) .

- Hili toleo lilifanya vizury sana sokoni , kutokana na upokelewaji wake . Hii ni kutokana na ushirikishwaj Wa kampun ya BMW kwenye mfumo Wa Umeme , hadi Leo nitoleo bomba sana.

#4 . Toleo la NNE ni mwaka
( 2012 - 2021).

#5. Toleo la tano nikuanzia ( *2022 - hivi Sasa )

Hili pia toleo zuri sana .

√ Range Rover ni aina ya Gari ambalo limetengenezwa katika ubora Wa hali ya juu , very classic na ni luxury vehicle ever.

√ Pamoja nakua ni very luxury ila hata kwenye hizi barabara zetu linapita , iwe sijui kwenye matope limekwama , kwenye majani kwamba itakua vigumu kushika brake haswaa wakati Wa umande .

√ ina shockup za upepo zinazosaidia Gari liwe level hatak**a kwenye miinuko , ukikanyaga jiwe .

√ kwenye viti kuna spika ndogo ambapo wakat umepumzisha kichwa unaweza kuskiliza na kuzuia kuskia kelele zozote .

Hizo tu ni miongoni mwa sifa za RANGE ROVER .
nyingi nyingi zitakujia hapa hapa , endelea kufuatilia.

Mtu Wangu! Usisahau Ku like na Kusave Post hii kwa ajili ya kutunza elimu hii!!!

IFAHAMU TOYOTA  PASSO.Mambo vipi mtu wangu Wa Nguvu πŸ’ͺ Leo bwana wewe, napenda kukuletea Gari pendwa ,Gari zuri Gari la k...
09/02/2023

IFAHAMU TOYOTA PASSO.

Mambo vipi mtu wangu Wa Nguvu πŸ’ͺ

Leo bwana wewe, napenda kukuletea Gari pendwa ,Gari zuri Gari la kuvimbia town _Toyota Passo_

Najua umeskia habary kulihusu ila hujaskia hii hapa :πŸ‘‡πŸ‘‡

1. Ni Gari zuri kwa mwonekano , zipo za kila rangi utakayo.

Pia tunatoa fursa yakukushauri rangi ipi nzuri kwa mazingira au matumizi yako.

2 . Inabana matumizi ya mafuta , ukilinganisha na Gari zingine,

Ukilinganisha na bei za mafuta kwa sasa itakusaidia kubana matumizi yako.

3. Ni rahisi kuifanyia maintenance ,haina gharama kubwa ,

Vifaa vyake vinapatikana mahali popote.

4. Ni rahisi kuendesha, haiitaji nguvu wala haikupi shida haswaa ukiwa barabarani, sababu ni nyepesi na nirahis kueleweka.

5.kwa matumizi yako yakutoka hapa napale ni Gari zuri sana litakufaa

Note: kwa kuwa tunatofautiana ya kimatumizi ,Toyota passo wakaja na suluhisho.

Passo zipo:

β€’ Masafa ya mbali ( piston 4 )

β€’ masafa ya karibu ( piston 3 ) na kuzifaham ni rahisi sana kwa kuangalia capacity ya engine yako.

β€’ kwa ushirikiano Wa kampuni ya Toyota na Daihatsu motor's. Wakafanikiwa kuingiza sokoni kwa Mara ya kwanza mwaka (2004 - 2018)

β€’ ilipata mafanikio mazuri hadi hivi sasa kwa ufanyanyi gazi wake.

Ni hayo kwa leo stay tuned, mengine mazury yatakujia 😊 πŸ‘

Follow | Comment | Like | Zaidi sana SAVE POST HII....

*NISSAN   DUALIS* Hellow habary ! 😊Katika STORY LEO!!!Napenda kukuletea  Gari aina ya Nissan, lenye ndugu wengi k**a Nis...
07/02/2023

*NISSAN DUALIS*

Hellow habary ! 😊

Katika STORY LEO!!!

Napenda kukuletea Gari aina ya Nissan, lenye ndugu wengi k**a Nissan extrail, Nissan juke , Nissan civilian, Nissan sunny n.k pamoja na Nissan Dualis.

Leo Tunamzungumzia hasaa Nissan Dualis.

Nissan ni miongini mwa kampun iliyokua inaongoza na kufanya vizury tangu mwaka 1933 nakushika nafasi ya 6 kwa ushindani ulimwenguni, ambapo awali ilikua ikifahamika k**a DATSUN kwenye masoko ulimwenguni.

Nissan Dualis vilevile inafahamika k**a Nissan Qashqai. ni kutokana na kabila la uajemi lililofahamika k**a qashqai maeneo ya milimani kanda za kusini na kati ya IRAN.

Jina la Nissan Dualis hutumika kwa nchi ya Japan na Australia ....lakini mahali pengine huuzika k**a Nissan Qashqai k**a uingereza nanchi zingine . muundo wake unafanana k**a Dualis.

β€’ Mnamo mwaka (2006 - 2013 ) J10 Nissan ilitoa toleo lake kwanza

β€’ Toleo la pili ( 2013-2021) J11

β€’ Toleo la tatu
( 2021- hivi sasa ) J12.

Generally

Nissani Dualis nigari nzury sana kwa luxury ,vilevile ina space kubwa ndani ,inaroof iliyotulia na ni nzury .vilevile ina seats za watoto kukalia.

Inafaa kwa safari zako zahapa napale na inauwezo Wa kwenda mbali sana . yaani masafa ya mbali .

Ina speed nzuri na imetulia barabarani wala haina mambo mengi.

SUBARU  FORESTERSubaru _Forester_ k**a Jinalake lilivyo . Nigari la luxury na pia linahimili mikiki mikiki ya barabarani...
04/02/2023

SUBARU FORESTER

Subaru _Forester_ k**a Jinalake lilivyo .

Nigari la luxury na pia linahimili mikiki mikiki ya barabarani.

Historia yake kwa ufupi

β€’ Subaru ilianza kutenganezwa kwa Mara ya kwanza kabisa mwaka ( *1997- 2002* ) SF ikiwa ni toleo la kwanza

β€’ Toleo la pili ( 2002- 2006) SG

β€’ Toleo la tatu (2008- 2013) SH

Hili ni miongon mwa toleo lilofanya vizuri kweli ,kutokana na highperfomace yake ya engine.

Uwezo wa kubeba vitu vingi na bado ikatulia barabarani na kua na speed ileile bila kuathiri chochote, ukiwa ndani huwezi kusikia sauti ya nje, ipo very comfortable.

Toleo la Nne (2012- 2018) SJ

Toleo la Tano (2018-2022) SK

Natoleo la sita litatoka mwaka huu . hizo hapo juu πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘† ni matoleo mbalimbali za forester!

😍 IN GENERAL
Subaru ni Gari Inayoweza kwenda masafa ya mbali zaid bila kupumzika njiani na bado ikadai safari.

Mfano ukatoka dar hadi Kenya, dar - mbeya bila kuipumzisha, ni imara zaidi.

● Mahali popote inapita, kwenye rough road zetu hizi , barabara za mashimo ,zina shockup imara ambapo hata ukiwa unaendesha usipate mitikiso yoyote.

● Ni rahis kuitumia kwenye dashboard yake imewekewa kila sign vizury zitakazo kuelekeza kwa urahisi.

Unaweza kubeba vitu vingi au watu wengi zaid , maana kua unaweza kunjua adi siti za nyuma na watu wakapata kukaa.

●Vilevile ni 4WD ni (four wheel drive) kwenye matope au k**a umekwama mahali nirahisi kutoka.

Kwa wale wanapenda safari ni gari nzuri kwa kusafiria wala haichoshi.

Comment, Like, Share na Save post hii kwa ajili ya kujifunza hapo baadaye!

Utapenda KUSIKIA habari za gari gani? Tuandikie hapo chini.. 🚘

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FirstCar Motors posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share