23/09/2020
UKAGUZI WA GARI
KUTOKA IHET DRIVING SCHOOL
Na Mr.Christopher Nuhu. Mtaalam na Mshauri wa vyombo vya moto (magari, bajaji,pikipiki na mitambo mizito-Heavy Equipments)
IHET Driving School iliyosajiriwa kisheria inatoa huduma bora kabsa za udereva wa magari, bajaji na pikipiki pamoja na kusaidia upatikanaji wa leseni kwa wanafunzi wake watakaohitaji kwakufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka ndani ya muda mfupi.
Huduma zetu hutolewa kwa gharama nafuu sana. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0715425429 au fika katika ofisi zetu zilizoko Sayansi katika kanisa la KKKT-Kijitonyama ghorofa ya 8, Dar es salaam, Tanzania
Tafsiri nyingi zinasema, gari ni chombo cha moto kinachotembea kwenye nchi kavu na chenye uwezo wa kuzalisha nguvu yake ili kuweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kutokana na tafsiri hii, na mara zote huundwa na sehemu kuu mbili yaani bodi pamoja na 'chasis' bodi ni ile sehemu inayofunika gari ambayo hufanya kazi za kubeba abiria na mizigo kutegemea na kusudi la kuundwa kwake, mara nyingi tunazo bodi za aina mbali mbali katika magari mfano tumezoea kusikia 'saloon' ambayo ni moja ya muundo wa bodi unaotumiwa na moja ya magari madogo, yako mengi yakuzungumza juu ya bodi lakini kwakuwa hii sisehemu ya lengo letu kwa mada hii nitatafuta muda nitaichambua kwa kina ili msomaji uweze kuwa na uelewa mpana zaidi.
Sehemu ya pili ya gari yaani 'chasis' ni sehemu kuu inayounda gari na kwa tafsiri rahisi unaweza kuita ni 'gari bila bodi' kwa maana kwamba ukiondoa bodi kwenye gari kinachobaki kiujumla wake huitwa chasis, ikumbukwe tu kwamba si gari zote hasa gari za toleo la siku hizi nyingi zimeundwa kiasi ambacho huwezikutenganisha sehemu hizi mbili labda kwakuharibu tu.
Katika chasis tunaomfumo maalum unaolifanya gari liwe tofauti na vyombo vingine vya usafiri kwakuzalisha nguvu yake binafsi, mfumo huu huitwa injini ambao ndo hufanya kazi ya kutengeneza nguvu yake kwa kushirikiana na mifumo mbalimbali iliyotengenezwa katika mfumo huu wa injini mfano mfumo wa uchomaji, mafuta, hewa, ufuaji umeme n.k baada yakuzalishwa nguvu hiyo husafirishwa kutoka kwenye injini kupitia mifumo mbalimbali mpaka kwenye matairi ya kuendeshea yaani 'driving wheels' na hatimae gari huweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Ndugu zangu, gari ni chombo kilichoundwa na mifumo mbalimbali ambayo hufanya kazi tofauti kwa ushirikiano ili kutimiza kusudi lililokusudiwa ktk gari hilo baadhi tu ya mifumo hiyo pamoja na niliyokutajia tunayo mingine k**a mfumo wa breki, mneso/suspension, taa n.k. Ili gari liweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi ni jambo la muhimu sana kuhakikisha mifumo yote iliyoko kwenye chombo hiki haina hitilafu ya aina yeyote sawasawa na binadamu tu kwamba akitokea hata kidole hakiko sawasawa basi ufanisi wake huathirika kutokana na kiungo hicho kuwa tu hakiko katika hali iliyozoeleka. Kwa maneno mengine, mifumo yote iliyowekwa ktk gari ni lazima kuhakikisha kila mmoja unawajibika sawasawa kutimiza kusudi lake.
Ili kuhakikisha mifumo hii inafanya kazi sawasawa, dereva au mtumiaji yeyote wa chombo hicho anawajibika kufanya ukaguzi katika chombo chake kwakupitia mfumo mmoja baada ya mwingine kwakuzingatia maelekezo ya mtengenezaji wa gari kupitia kitabu cha mwongozo (manual guide book) ambao unakuwemo ktk kila gari.
Aidha ukaguzi umegawanyika ktk makundi makubwa mawili yaani ukaguzi wa kisheria ambao huu hufanyika kwa mjibu wa sheria zilizoweka, ukaguzi huu huhusisha uangaliaji wa bima, kadi ya gari, leseni ya dereva n.k na mara nyingi tumekuwa tukishuhudia ukifanywa na askari wa kitengo cha usalama barabarani.
Kundi la pili ni ukaguzi wa kiusalama na mara zote huu hufanywa na dereva, mmiliki au mtaalamu aliyeidhinishwa kuwa na sifa zinazokubalika ktk kulikagua gari na hata kufanya matengenezo ingawa kutokana na hali halisi ya ukosefu wa chombo maalumu cha kuratibu wataalam hawa tumekuwa tukishuhudia kazi hizi zinafanyika kiholela na hata kuongeza matatizo hasa ktk magari ya toleo la siku hizi ambayo kimsingi yanatumia teknolojia ya juu mno.
Ukaguzi huu wa kiusalama unalenga kuhakikisha wakati wote mifumo yote iliyopo katika gari inafanya kazi kwa ufanisi unaokubalika kadri ya maelekezo ya mtengezaji wa gari husika na ieleweke kwamba ukaguzi huu umegawanyika katika makundi makubwa mawili yaani ukaguzi wa kila siku na ukaguzi wa mda maalum.
Makundi haya mawili yamewekwa makusudi kabsa kwa kuzingatia aina na tabia ya mifumo iliyopo katika gari kwa mfano iko mifumo ambayo ikitokea hitilafu kidogo tu madhara yake yaweza kuwa makubwa sana hivyo kuweza kuepuka uwezekano wakutokea kwa madhara hayo ikaonekana ni vema kuwe na ukaguzi wa mara kwa mara ktk gari lako ili kujihakikishia usalama wake mfano tu wa sehemu zinazotakiwa kukaguliwa mara kwa mara ni pamoja na mfumo wa breki, matairi, ukaguzi wa jumla wa nje ya gari lako, kuangalia k**a kuna majimaji yamedondoka chini mfano maji ya kupozea, oili ya injini, mafuta ya usukani, oili ya gear box, difu n.k
Kundi la pili huhusisha ukaguzi wa mda maalumu kwakuzingatia umbali wa gari liliotembea, ieleweke tu kwamba kila kipuri(spare part) kilichofungwa ktk gari kina mda maalum wakutumika kikiwa na ubora wake na baada ya hapo inashauriwa ukibadilishe au ufuate ushauri ulioelekezwa na mtengenezaji wa gari husika. Changamoto kubwa iliyopo kwa watumiaji wengi wa magari wamekuwa hawana tabia yakubadilisha vipuri vya magari yao mpaka utokee uharibifu hali ambayo mbali na kuongeza gharama na mda wa matengezo pia imekuwa ikiongeza uwezekano wa kuhatarisha maisha ya watumiaji wengi wa vyombo vya moto. Ikumbukwe kuwa kuelewa maeneo ya kukagua kila wakati na kwa wakati maalum na mbinu sahihi na nini chakukagua ktk kila eneo ni jambo la muhimu sana kuelewa kila mmoja wetu.
Ndugu zangu, ziko faida nyingi sana za kuzingatia taratibu za ukaguzi wa gari, ikiwemo kukuepusha na uwezekano wa kupata ajali inayotokana na uharibifu wa gari lako, sababu ambayo bado imeonekana kuwa changamoto katika nchi yetu. Tatizo ambalo linaweza kukomeshwa bila gharama yeyote zaidi ya kuelewa tabia za gari lako na kufuata maelekezo ya mtengenezaji. Mimi kila mmoja wetu achukue hatua kuanzia unapomaliza kusoma makala hii, ili tuweze kuwa na uelewa wa pamoja katika kipengele hiki muhimu cha ukaguzi, kwa wasio na elimu hii usisite kuwasiliana nasi kuweza kupata mafunzo haya ili uwe balozi muhimu wa kulinda usalama wa chombo chako. Ahsante!
K**a una ndugu, jamaa na rafiki na ungependa aweze kupata umahiri wakuendesha gari, bajaji ama pikipiki, IHET DRIVING SCHOOL ipo kwa ajiri yako, Huduma zetu ni kukuwezesha uweze kufikia malengo yako yakuwa dereva mahiri na mwenye vigezo kisheria, shule itasimamia pia zoezi la upatikanaji wa leseni watakaohitaji kwakuzingatia taratibu zilizowekwa na mamlaka kwa mda mfupi zaidi, Piga simu au WhatsApp 0715425429 kupata maelezo zaidi.
Huduma zetu zinatolewa kwa gharama nafuu na utahudumiwa wakati wowote na popote ulipo
Fika ofisini kwetu Tunapatikana, Sayansi kijitonyama, katika kanisa la KKKT-Kijitonyama Ghorofa ya 8, Dar es salaam, Tanzania
Contact us IHET DRIVING SCHOOL
FACEBOOK PAGE: Ihet driving school
Call:0715425429
WHATSAP:0715425429
WEBSITE: www.ihet.ac.tz