Bernard Msirikale

Bernard Msirikale Q&R REAL ESTATE INVESTMENT
Tunavyo Viwanja na Mashamba kwa Bei nafuu. Bagamoyo,Kibaha-Boko, Mlandizi

05/11/2025
03/11/2025

HATUNA VYOMBO VYA HABARI

Kwa hakika mimi binafsi nimesikitishwa na utendaji wa vyombo vya habari vya hapa nchini hasa redio na runinga.

Vyombo (vyao) vyote vya habari vilikuwa kimya kwa matukio yaliyotokea mara baada ya kile kilichoitwa uchaguzi.
Habari za uharibifu wa mali za chama tawala, serikali (umma) na pia watu binafsi hazikutolewa tangu kutokea kwake hadi leo mara baada ya kutangazwa viongozi wateule.

Hata hivyo bado pia vimeshindwa kutueleza ni maafa kiasi gani yaliyotokea.
Je, ni raia wangapi wameuawa na kujeruhiwa?
Je, ni askari wangapi pia wamepoteza maisha na kujeruhiwa?

Inakuwaje mambo au matukio yaliyotokea hapa nchini kwetu yatangazwe na vyombo vya habari vya nje ilhali vya hapa kwetu viko kimya?
Inakuwaje mambo au matukio yaliyotokea jana nchi jirani yatangazwe leo tena na vyombo vyetu vya habari?

Je, hayo matokeo ya ushindi na pongezi wanazoendelea kututangazia leo, ndiyo mambo muhimu kwao na kwetu kuliko hali, mali na maisha yetu Watanzania?
Je, Amri na Maagizo ya kutotangaza hayo matukio yalitoka kwa nani?
Je, kuna sababu zipi za maana za kuficha habari hizo muhimu?

30/10/2025

UCHAFUZI
Ni dhahiri kuwa tume na serikali ya CCM huwa na nia ovu dhidi ya chama kikuu cha upinzani - CHADEMA.

Mwaka huu hatukuona wala kusikia kuwa kuna mgombea udiwani yeyote wala mgombea ubunge ambaye jina lake likikatwa kutokana na sababu yeyote ile.

Pia kuwa hakuna msaidizi wa uchaguzi yeyote yule ngazi ya kata wala wilaya waliozikimbia ofisi zao ili wagombea washindwe kurejesha fomu zao k**a ilivyotokea miaka iliyopita kwa wagombea wa CHADEMA.

Je, hayo yametokea kwa bahati mbaya?
Au pia huwa ni mipango haramu yao tu?

Huo ni uthibitisho usio na shaka kuwa kumbe tatizo lao kubwa si utaratibu au ujazwaji wala muda bali ni CHADEMA tu na si vinginevyo.

30/10/2025

VYOMBO VYA DOLA
Leo kumetokea mkanganyiko usio wa kawaida kati ya vyombo vyetu vya dola.Sisi k**a taifa na wananchi kwa ujumla tumejifunza nini?

Wakati wa maandamano yaliyofanyika leo, utofauti uliojitokeza kati ya polisi na jeshi la wananchi limekuwa ni tukio la kushangaza k**a siyo la kutia aibu.
Yaani wakati polisi wetu wakitumia bunduki na risasi za moto kuwatawanya na kuwak**ata waandamanaji, wao JWTZ walikuwa wakipita tu barabarani kuangalia usalama na kuimarisha ulinzi bila hata kuwazuia watu waliokuwa wanaandamana.

Tukio hili lilishangiliwa sana na waandamanaji wenyewe na pia hata kuwashangaza watu wengine waliokuwa wakishuhudia.

Je, hivi limetokea kwa bahati kwa mbaya?
Je, kwanini hali imekuwa tofauti hivi?

30/10/2025

VYOMBO VYA HABARI
Ni takribani miezi mitatu hivi ya kampeni vyombo vyote vya habari hususani redio na runinga vilikuwa msitari wa mbele kutuhabarisha mwenendo wa kampeni na kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Lakini ni jambo la ajabu lisilokuwa la kawaida leo hii, vimeshindwa kututangazia juu ya maandamano ktk mikoa mbalimbali na tafrani iliyojitokeza ikiwa ni pamoja na mauaji yaliyofanywa na polisi dhidi ya raia.

Hadi mida hii ya usiku, vyombo vingi k**a si vyote viko kimya tu juu ya matukio hayo na vimekatiza vipindi vyao vya kawaida huku vikipiga miziki na nyimbo za amani.
YAANI NI K**A VINAKUMBUKA SHUKA ILHALI KUMESHAKUCHA

03/06/2024

Address

City Centre
Dar Es Salaam

Telephone

+255784789878

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bernard Msirikale posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Bernard Msirikale:

Share

Category