21/03/2024
Tofauti ya hizi gari kati Alphard G na V ukiachana na ile nembo inayobandikwa nyuma, ni kwenye "grille"(facelift) za mbele.
Mfano kwenye picha ukiangalia facelift ya Alphard G na V old, "G" ina vimstari vimstari vingi(chrome) vilivyosimamama alafu ina mistari miwili tu mikubwa ya grille iliyolala ambayo imekatisha juu kwenye hivyo vimstari vidogo vilivyosimamama. Ila ukiangalia "V" ina mistari minne mikubwa iliyolala(horizontal) na mistari mitano iliyosimama.
Kwenye model mpya za facelift ya Alphard, kuna mabadiliko kidogo kwenye idadi ya mistari ya grille kwa model zote mbili. Alphard G new model ina mistari ya grille mitatu mikubwa iliyolala(horizonatal) na miwili ikiingiliana na logo. Na hapa ina vimstari vidogovidogo vingi ila ni k**a vimelala kidogo kuelekea katikati.
Alphard V imekuja na mistari iliyolala miwili(horizontal) na mitano iliyosimama(vertical) na ni minene kidogo ukilinganisha na facelift ya old.
Alphard G na V zinasambazwa na wauzaji wawili tu Japan ambao ni Netz na Toyopet. Toyopet yeye anasambaza model za Alphard G, na Netz anasambaza model za Alphard V. Hatahivyo, utakapoona Alphard nyuma zimebandikwa sticker ya "Yokohama Toyopet" fahamu kuwa hiyo ni Model ya G inayosambazwa na wauzaji wa Toyopet, Yokohama.
KUMBUKA: Kuanzia generation ya pili ya Alphard, Toyopet wanasambaza Toyota Alphard tu, na Netz wanasambaza Vellfire.
Ramadan Kareem!