07/05/2026
1. Taa ya Oil Pressure kuwaka — Simamisha gari mara moja na zima engine. Kila sekunde unayoendelea kuendesha, chuma kinakwangua chuma ndani ya engine. Kupuuza tatizo hili kunaweza kuharibu engine kabisa.
2. Taa ya Temperature kuwaka — Zima AC mara moja na washa heater kwa kiwango cha juu kusaidia kupunguza joto la engine. Ukiendelea kuendesha bila kufanya hivyo unaweza kuunguza head gasket.
3. Taa ya Battery kuwaka — Alternator inaweza kuwa imeharibika. Gari linaendelea kutumia umeme uliobaki kwenye battery tu, hivyo linaweza kuzima muda wowote hata ukiwa barabarani.
4. Taa ya Brake kuwaka — Inaweza kuwa brake fluid imepungua au mfumo wa brake una hitilafu. Usipuuzie hii, brake zinaweza kufeli ghafla.
5. Check Engine Light ikipepesa (flashing) — Hii ni hatari. Simamisha gari mara moja kwani inaweza kuharibu catalytic converter na kuongeza gharama kubwa za matengenezo.
Ukikutana na changamoto hizi au nyingine zinazofanana, tupigie au tutumie ujumbe kupitia namba zilizo hapa chini tukusaidie kujua tatizo na hatua sahihi za kuchukua mapema.
Tutakujibu haraka iwezekanavyo.
📞 Tupigie:
0222630166
🕢 Kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 1:30 usiku kila siku
📱 0628555566
(WhatsApp Text & Calls pamoja na simu za kawaida)
⚠️ Tafadhali usitume SMS za kawaida kwani hatutaziona.
🕐 Huduma masaa 24/7 kila siku
📍 FirstStop — Tawi la Tegeta & Tabata
: