05/06/2026
Arusha Auto Show For Everybody!
Arusha Auto Show inakupa fursa kuona kazi za watu, vilevile kuonesha kazi zako.
'Kazi' ni kazi zinazohusiana na mambo yote ya magari - maana halisi ya "Maonesho ya Magari Arusha"
Ikiwa wewe ni fundi, mmiliki wa gari, mshabiki ama mfanyabiashara, hapa ndio mahali pako.
Kutana na wenzako, jifunze mambo na vitu vipya, pata Hamasa na ari mpya, tengeneza 'network' na watu wa aina yako - wapenda-magari.
Arusha Auto Show ni kwaajili ya kila aina ya gari, haibagui, haichagui - unaweza sema Arusha Auto Show For Everybody!
Tarehe ni ile ile
Septemba 5 - 6, 2026
Magereza Grounds - Kisongo
Tembelea π www.arushaautoshow.com
πΈ .nunes05