Muba mzee baba

Muba mzee baba Laailaha illalwah

30/01/2022

Acheni majungu kazi zipo tuu

Ipo sokoni inauzwa toka ije ina wikii 3 mfumo wa wa kugandisha  inagandisha vizuri  mawaliano 0716172784
07/02/2021

Ipo sokoni inauzwa toka ije ina wikii 3 mfumo wa wa kugandisha inagandisha vizuri mawaliano 0716172784

07/02/2021

Dawa ni kujifujiza tuuuuu ni bora selikali ianzishe siku ya kujifujiza km ilivyo siku ya usafi

31/12/2020
02/07/2020

Mume wangu naomba leo usinipige, nimechoka sana mume wangu, naomba tu usinipige…” Mke wangu aliongea kwa unyonge, alikua amekaa sebuleni kachoka, mimi ndiyo nilikua nimetoka kazini. “Inamaana unaniona mimi mjinga nakupiga tu bila sababu, k**a umefanya kosa utapigwa tu mpuuzi mkubwa! Yaani mume wako anarudi kutoka kazini badala ya kumpokea unaanza kuongea habari za kupigwa! Mbwa mkubwa wewe! Shetani wewe, unataka nijisikie vibaya kuwa nakupiga piga bila sababu!” Nilijikuta nawaka, sijui hasira nilizotolea wapi lakini mke wangu alinitibua, kwa maneno yake nilimfuata na kutaka kumpiga.
Tofauti na siku nyingine mke wangu alikua amekaa tu, nilimsogelea mpaka alipokua kakaa, nikamshika nguo yake na kumnyanyua huu, nilishangaa alikua mwepesi sana, lakini sikujali, nilimsukuma na kumkanyaga tumboni, nik**alizia kwa matusi kadhaa kisha nikaingia zangu ndani. Hakunyanyuka pale alipokua amekaa na wala hakupiga hata kelele. Sikua nimepanga kutoka, lakini niliona k**a mke wangu amenikosea heshima, kaniharibia siku yangu, nilitoka na kumpita pale sebuleni, sikumsemesha kwani nilikua na hasira, nilienda mpaka mezani na kuchukua ufunguo wa gari, gari ya mke wangu.
Ingawa ilikua na jina langu lakini ilikua ni gari ambayo mke wangu alinunua kwa pesa zake lakini baadaye nilimlazimishia akabadilisha jina na kumpa. Nilikua nikiitumia k**a yangu, alinunua kwaajili ya kuendea kazini, wakati huo sina kazi lakini nilikua nazurura nayo kufanya umalaya. Hata nilipopata kazi na kuwa na gari la kazini lakini bado nilimnyanyasa, sikumruhusu kuendesha na k**a ikitokea anaendesha nilikua nampiga sana. Niliondoka mpaka kwa Mama mmoja mtu mzima ambaye alikua ni mchepuko wangu wa muda mrefu, naye alikua ananihudumia na mara nyingi alikua akimpigia simu mke wangu kumtukana.
Mimi ndiyo nilikua namuambia, ampigie kumtukana ili mke wangu ajue kuwa mimi ni kidume na si k**a yeye anavyonidharau. Kila siku nilikua naamini kuwa mke wangu ananidharau ndiyo maana nilikua namdhalilisha kila siku. Usiku nilipigiwa simu, ilikua k**a saa nane usiku, ilikua ni simu ya Mama yangu, nilishangaa na kuhisi kitu kibaya kimetokea, Baba yangu alikua anaumwa ana hali mbaya Kijijini, nilijua k**a Mama ananipigia simu usiku huo basi labda ameshafariki.
“Uko wapi?” Mama aliniuliza baada ya salamu. “Acha upumbavu, watu wanakutafuta haupatikani, simu umezima ya nini? Inamaana huna taarifa za msiba?” Nilishangaa, simu yangu sikuzima kabisa lakini Mama alikua anasema sipatikani, alitaja msiba nikajua Baba tayari, lakini kwa namna alivyokua anaongea Mama nik**a hakuna kitu kimetokea kikubwa. “Baba amefariki?” Niliuliza kwa kusikitika, nilijifanya kushangaa lakini ukweli ni kitu ambacho wote tulikua tunakisubiria. “Chunga na mdomo wako! Tema chini! Mama Sadia, Mke wako kafariki! Yaani unasema upo nyumbani hata hujui k**a mke wako kafariki?” Nilishikwa na butwaa kwani nilikua sijui chochote.
“Nitakua nimemuua mke wangu!” Niliwaza huku nikinyanyuka na kuvaa nguo, Mama bado alikua anaongea lakini sikujua hata anaongea nini? Niliwaza mambo mengi, niliwaza kuhusu Polisi, nilijua ni mimi, niliwaza labda nilimkanyaga vibaya, niliwaza kuhusu mwanangu Sadia, ndiyo kwanza alikua na miaka mitatu. Baada ya kukaa kwenye ndoa bila mtoto nilishakata tamaa mpaka nilipompata Sadia, kwanza mke wangu alipopata ujauzito nilijua si wangu, nilikua nampiga sana ili mimba itoke lakini Mungu aliniumbua, alikua ni mtoto wakike lakini alifanana kila kitu na mimi, hata ningekataa vipi isingeeleweka.
Nilikua na wasiwasi kuwa si wangu kwani tangu mdogo nilikua na tatizo la nguvu za kiume, nilikua siwezi kufanya mapenzi kwa zaidi ya dakika mbili, nalala na hata goli langu lilikua dhaifu, nlishahangaika kwa waganga mahospitalini kimya kimya kote naambiwa mbegu zangu hazina nguvu. Pamoja na kuujua ukweli lakini siku zote nilikua namshutumu mke wangu, namuambia yeye ndiyo mwenye matatizo nampig na niligoma kabisa kuongozana naye hospitalini, alipopata ujauzito niliukana kwani niliambiwa siwezi kupata mtoto kirahisi kwakua mbegu zangu hazina nguvu.
Nilipewa madawa mengi lakini kila nikipima niliona k**a hayasaidii, nikaamua kuacha na kuhamia kwenye pombe na wanawake ili kujiona kidume. Baada ya mke wangu kujifungua mwanangu niliacha manyanyaso kidogo, ndoa ikawa na amani lakini nilshazoea, nilikua sina raha, nilikua nahisi kwakua sina nguvu za kiume labda ananidharau, labda ana wanaume wengine, nilikua nampiga sana bila sababu, yaani hata k**a akinifumania mimi, kosa ni langu lakini nampiga, sasa alikua amekufa, nilikua nimemuua.
Yule Mama niliyekua natembea naye aliniuliza, nilimwambia mke wangu amekufa kisha nikaondoka. Nilienda mpaka nyumbani nikiogopa, nilimpigia dada wa kazi, alikua analia tu, nikamwambia amtoe mtoto nje naenda kumchukua. Lengo langu lilikua ni kumchukua mwanangu na kutoroka naye, kwangu ilikua bora kuondoka kuliko kesi ya mauaji. Kila mtu alikua anajua kuwa nampiga mke wangu na nilijua dada wa kazi kaona nikimpiga hivyo k**a Polisi wakija basi atahojiwa na mimi nitak**atwa.
Nilifika nyumbani lakini Dada alikua bado hajatoka, niliangalia kulikua na watu wachache, nilitaka kuondoka, lakini kabla ya kufanya hivyo waliniona na kuanza kunipa pole, pamoja na kuwa ilikua usiku watu walikua wanakuja nyumbani kwangu. Nilingia nao, mke wangu alikua chumbani, niliingia na kumuita k**a vile kalala. “Kansa mbaya sana, yaani ziwa lote limeoza, Pole Kaka yangu, mimi sikujua…” Alikua ni Dada yangu, mimi mwenyewe sikujua k**a mke wangu anaumwa, niliitikia pole yake na kumuambia atoke nataka kubaki na mke wangu.
Alitoka na kuniacha peke yangu, nilimfuata mke wangu kitandani, nikaamfunua t**i moja la kulia lilikua lina k**a limeisha flani, huku jingine likiwa limeoza lakini si sana. Nilishangaa kwani ni muda sana sijamgusa mke wangu, tangu ana ujauzito wa mtoto wetu niliacha kutembea naye mpaka alipojifungua. Nilikua namuambia kuwa ananuka, ameharibika hanivutii lakini ukweli nikuwa nilikua siwezi kufanya mapenzi, hata kwa michepuko mingi niliishia kuilewesha na kuishikashika, sikua na hisia na sikua na nguvu kabisa, hata zile dakika mbili nilikua siwezi tena.
Kumbe baada tu ya kujifungua mke wangu aligundulika kuwa ana Kansa ya t**i, alishafanyiwa upasuaji lakini haikusaidia, wakati huo mimi nilikua hapohapo nyumbani lakini sikujua kuwa mke wangu alishawahi kulazwa hospitalini mwezi. Mara nyingi tu nilikua sirudi nyumbani na kumbe alikua akiwadanganya watu nimesafiri kikazi ili kulinda ndoa yake. Aisee nilipata mwanamke, niliumia sana siku anazikwa, kumbe siku ile ananiambia nisimpige nikuwa alikua anataka kufa kwa amani, mke wangu alifariki nikiwa sijui k**a anaumwa.
Ndugu walinipa pole, majrani waliniangalia tu kwani walikua wanajua tabia zangu lakini hakuna ndugu hata moja ambaye alijua. Walikua wananilindia siri yangu. Ni mwaka wa kumi sasa tangu mke wangu kufariki, sijaoa mwanamke mwingine, sio kwamba sitaki lakini siwezi, kila mwanamke nineyekua naye nikitembea naye kidogo ananiacha, nina msongo wa mawazo. Wakati Mama yake anafariki mwanangu alikua na miaka mitatu, lakini huwezi amini tangu siku hiyo mwanangu hajakubali nimguse, huwezi amini ni k**a alikua anaona mambo yote niliyokua namfanyia Mama yake.
Nakumbuka ilikua ni baada ya kutoka makaburini, mwanangu alikua analia, watu wakasema mpelekeni kwa Baba yake, walimleta, alilia mara kumi yake, huku akipiga kelele “Hitaki! Sh*taki! Sh*taki!” Aliongea huku akilia na kujirusha, tangu siku hiyo hakukubali kabisa nimguse. Sasa hivi ana miaka 13, anasoma Dadasa la 6 lakini hanipendi, ananichukia k**a vile si Baba yake, Mama yake angekua hai au angekufa akiwa mkubwa ningesema kamwambia mambo mabaya, lakini si hivyo ananichukie tu. Nafanya kazi, nina kipato kizuri lakini maisha kwangu hayana thamani, sijaoa, nasingizia bado nina uchungu wa mke wangu kumbe nina mengine.
Lakini nawaza je naweza kupata mwanamke mwingine k**a mke wangu, pamoja na kujishusha, kujaribu kunipa furaha lakini sikuiona, nilibaki na maumivu yangu tu. Maisha yamekua magumu sana kwangu, natamani kurudisha siku nyuma, angalau niishi kwa amani na mke wangu, nimuonyeshe hata nusu tu ya mapenzi ambayo alikua ananionyesha lakini siwezi, najuta na sijui cha kufanya. K**a una mtu anakupenda na anakuonyesha upendo basi muonyeshe kwelikweli kwani muda wa kuishi hapa duniani ni mchache sana, acha kutumia kwa kuwa na kisirani.
MWISHO

22/06/2020

Address

Daima Garage
Kawe

Telephone

+255716172784

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Muba mzee baba posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Muba mzee baba:

Share