Jiefang Motors Tanzania

Website

Jiefang Motors Tanzania sell faw trucks in Tanzania( Tipper ,Tractor Head, Cargo Truck)

28/01/2026

Kampuni ya JIEFANG ( Jiefang Motors Tanzania) inayohusika kutengeneza Magari ya mizigo ya FAW, imeendelea kumtambulisha mnyama wake hodari wa mizigo aitwae J5P 380HP 6ร—4, gari la mizigo lililobuniwa mahsusi kukidhi mahitaji ya usafirishaji wa mizigo mizito katika mazingira ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Trekta hii inaendeshwa na injini ya WEICHAI WP10.380E32 yenye nguvu ya 380HP ikiwa na uwezo mkubwa wa kuvuta mizigo mizito kwa safari ndefu kuelekea mikoa k**a Dar es salaam, Arusha, Mwanza na maeneo mengine yenye miinuko na barabara za changamoto.

Kwa upande wa usalama na uimara, J5P 380HP imefungwa na mfumo wa breki wa WABCO (ABS na vali) unaosaidia kuimarisha udhibiti wa gari hasa katika mteremko mrefu ambapo Lori hili lina sehemu ya mbele ya chuma tupu (all-steel front end) inayostahimili matumizi katika barabara mbovu na maeneo ya kupakia mizigo, matumizi ya betri zisizohitaji matengenezo hupunguza muda wa gari kusimama kazini.

Kwa ufanisi wa safari ndefu, trekta hii imewekewa tenki la mafuta lenye uwezo wa lita 600 linalowezesha safari ndefu bila kusimama mara kwa mara kujaza mafuta na uwezo wa kubeba mzigo wa kilo 41,300 (GCW) na chassis imara ya 6ร—4 yenye uwezo wa kusafirishaji makontena, mizigo ya jumla na bidhaa nzito hivyo kuongeza tija na mapato kwa Wamiliki wa magari na makampuni ya usafirishaji.

Kwa mujibu wa FAW Tanzania yenye makao yake TAZARA, Dar es salaam, wanunuzi wa trekta hii watanufaika na waranti ya miezi 12 kwa gari lote na waranti ya miaka miwili kwa mfumo wa power chain ikiwemo clutch, gearbox, axle na cab housing, tembelea Makao Makuu ya FAW Nyerere Road (Mkabala na TAZARA), Dar es salaam

๐Ÿ“ž Simu: 0795 339 339

21/01/2026

Kampuni ya FAW Tanzania ( Jiefang Motors Tanzania) imeendelea kuimarisha sekta ya usafirishaji Nchini Tanzania kwa kuwaletea Watanzania gari la mizigo aina ya FAW J5K 180HP closed-body cargo truck, lenye uwezo mkubwa lililotengenezwa mahsusi kwa barabara na mahitaji ya biashara za Tanzania.

Gari hilo lina uwezo wa kubeba hadi kilo 18,000 (GVW) na lina box la mizigo lenye urefu wa meta 6.2 likiwa na ujazo wa karibu 32 cubic meters ambapo muundo wake wa closed-body hulinda mizigo dhidi ya mvua, vumbi na wizi hivyo kulifanya kufaa kwa usafirishaji wa bidhaa za biashara, mazao ya kilimo, vifaa vya ujenzi na bidhaa za viwandani.

FAW J5K 180HP linaendeshwa na injini ya XICHAI yenye nguvu ya 180HP, inayojulikana kwa uimara na matumizi bora ya mafuta huku tenki lake la mafuta likiwa na uwezo wa kuhifadhi lita 200 linawezesha safari ndefu za ndani na nje ya miji bila kusimama kuongeza mafuta mara kwa mara.

Kwa upande wa faraja, gari hili limewekewa Air Conditioning, kiti cha air suspension, pamoja na betri isiyohitaji matengenezo, hatua inayolenga kupunguza uchovu wa dereva na gharama za uendeshaji kwa Wamiliki wa biashara.

FAW Tanzania pia imetangaza dhamana ya kuvutia kwa wanunuzi, ikitoa mwaka mmoja wa warranty kwa gari lote na miaka miwili kwa mfumo wa nguvu (powertrain) ikijumuisha gearbox, axle na sehemu nyingine muhimu ambapo FAW J5K 180HP inalenga kusaidia wafanyabiashara, makampuni ya logistics na wasambazaji kuongeza ufanisi na faida kwa kusafirisha mizigo mingi zaidi kwa safari chache.

๐Ÿ“ Ofisi za FAW Tanzania zipo Nyerere Road (Opposite TAZARA), Dar es salaam pamoja na mtandao wa mauzo na huduma Nchi nzima. ๐Ÿ“ž kwa maelezo zaidi au ku-book test drive, piga 0795 339 339.

06/01/2026
27/11/2025

Ni miaka mitatu sasa tangu Kampuni ya kutengeneza Magari ya mizigo ya FAW ( Jiefang Motors Tanzania ) iliingize sokoni Nchini Tanzania gari lake aina ya J5K ambalo lililetwa mahususi kuziba nafasi iliyokuwa wazi ya hitaji la Wafanyabiashara wengi kuwa na Gari la mizigo la aina hii.

J5K ni Gari la mizigo lenye uwezo mkubwa wa kubeba mizigo na kuhimili mazingira magumu ya barabara za Afrika likiwa na tanki la mafuta lenye uwezo wa kuhifadhi lita 200, Air Deflector, Air Conditioning, kiti cha Air Suspension na betri isiyohitaji matengenezo.

Faida zake ni pamoja na nafasi kubwa inayopatikana ya kubeba mizigo pamoja na kuikinga kwa usalama dhidi ya mvua, jua au vumbi, faida nyingine ni urahisi wa upatikanaji wa vipuri vyake pamoja na ulaji mdogo wa mafuta unaowezesha Mfanyabiashara kutengeneza faida zaidi, tembelea Ofisi za JIEFANG MOTORS zilizopo barabara ya Nyerere mkabala na TAZARA Dar es salaam au wapigie kwenye 0795-339-339.

NEW J5P 290HP 6X4 Tipper - 15.5CBM  # FAW TRUCKS #
22/10/2025

NEW J5P 290HP 6X4 Tipper - 15.5CBM # FAW TRUCKS #

K**a biashara yako inahitaji lori lenye nguvu, uimara na uwezo wa kufanya kazi kubwa bila maumivu ya kichwa basi Lori hili la FAW aina ya J5P 290HP 6x4 ndilo jibu sahihi, wanaliita JITU LA KAZI lililotengenezwa mahsusi kwa mazingira ya Afrika, iwe ni kazi ya kwenye migodi au mtaani kwenye ujenzi, J5P inabeba mzigo mzito na kuchapa kazi kadri unavyoituma.

Nikiwa hapa Jiefang Motors Tanzania Makao Makuu maeneo ya TAZARA, Mtaalamu wao ananiambia injini yake ni WEICHAI WP10.290E32 na nguvu yake ni 290HP, ina uwezo wa kupanda milima, kusukuma mizigo mikubwa na kufanya kazi masaa mengi bila kupoteza nguvu huku muundo wake wa 6x4 drive matairi yote ya nyuma yanasimamia nguvu ya kutosha na msukumo iwe ni kwenye barabara ngumu au zenye matope.

Tipper yake ina ujazo wa 15.5 cubic meters (CBM) inaweza kutumika kubeba mchanga, kokoto, mawe, mizigo ya ujenzi au mizingo mingine huku ikitumia mfumo wa valves wa WABCO unaoongoza duniani kwa ubora wa breki na usalama hivyo kulifanya Lori hili kuwa ni mashine ya kutegemewa inayochanganya nguvu, teknolojia na ufanisi, kuhakikisha kila safari inaleta faida na mafanikio.

Kwa manunuzi au maulizo zaidi unaweza kufika Ofisi za JIEFANG MOTORS ( FAW) zilizopo Barabara ya Nyerere mkabala na TAZARA Dar es salaam au unaweza kuwapigia kwenye 0795 339 339.

09/10/2025

Naomba hii post kwa leo niwapendelee na iwe maalum kwa Ndugu zangu wanaofanya biashara ya mizigo kwa kutumia Malori na wale wenye mipango ya kuingia kwenye biashara hiyo iwe ni kwa masafa marefu au mafupi, kuna hili Lori la FAW aina ya JH5 380 ambalo lilianza kuuzwa Tanzania tangu mwaka 2021 na tangu wakati huo hadi sasa rekodi zake za mauzo ziko juu kupitia Jiefang Motors Tanzania

Zipo aina mbili za FAW JH5 380HP ambazo ni 'HEAVY' na 'LIGHT', heavy ina uzito wa chassis wa KG 8100, light KG 7800 hivyo kufanya zote kuwa nyepesi ukilinganisha na Malori mengine, zingatia kwamba chassis nyepesi k**a hizo zinachangia kuongeza ufanisi wa matumizi ya mafuta na kuongeza kasi ya usafiri bila kupoteza nguvu ya kuvuta huku uwezo wake wa mafuta katika matanki yake mawili ukiwa ni lita 1100 kwa jumla zikimuwezesha Dereva kutembea umbali mrefu bila kuongeza mafuta.

FAW JH5 380 ni lori lenye mfumo wa 6x4 ikimaanisha lina magurudumu sita, manne kati yake hupokea nguvu moja kwa moja kutoka kwenye injini ambapo huu muundo una muhimili mmoja wa kuongozea na mihimili miwili ya kuendesha gari kitu ambacho kinalifanya kuwa chaguo sahihi kwa kazi ngumu za usafirishaji.

Kwa maana hiyo basi k**a mishemishe zako zinahusu usafirishaji wa vifaa vizito, chuma, makaa ya mawe au mizigo ya umbali mrefu au masafa mafupi hili ndio Lori lako, usisahau pia uwezo wa Lori hili katika nguvu ya kuvuta na pia magurudumu manne ya kuendesha hutoa msukumo mkubwa unaozuia kuteleza kwahiyo sahau kukwakwama barabarani.

Makao Makuu ya FAW yaliyopo TAZARA Dar es salaam yametangaza kuwa Wateja watakaonunua Lori hili watakuwa na WARRANTY k**a ifuatavyo, dhamana ya mwaka mmoja (12 miezi) kwa gari zima, dhamana ya miaka miwili (24 miezi) kwa mfumo wa power chain unaojumuisha clutch, gearbox (nyumba na vipuri vya ndani), gearbox mounting, intermediate axle, rear axle housing, inter-axle differential, na cab housing, piga namba #0795339339 kwa maelezo zaidi.

03/08/2025

FAW trucks!! Customer pick up truck ,our contact 0795 339 339

New J5P Series 340HP 6X4 TIPPER - 19.32 CBM
22/07/2025

New J5P Series 340HP 6X4 TIPPER - 19.32 CBM

Address

P. O. BOX 40902, Nyerere Road (Opposite TAZARA)
Dar Es Salaam
P.O.BOX40902

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jiefang Motors Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category