06/06/2026
hii inamaanisha kwamba;
1. hizi gari zinazotumia mafuta (petrol na dizeli) nyingi zitatupwa afrika kwa bei rahis sana, ili hawa watengenezaji wafidie baadhi ya pesa walizo wekeza katika uzalishaji wa magari na engine za mafuta
2. hizi gari za mafuta za bei rahisi sasa zitajaa afrika, kwa maana hiyo afrika ita kuwa muharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na wingi wa magari ya mafuta ambayo huzalisha carbon dioxide.
sasa zile taasisi za dunia zinazo husu mazingira zitaingia na kuishutumu afrika kwa uharibifu wa mazingira.
3. Afrika kwasababu huwa tunafuata tu kila kisemwacho na taasisi hizi, basi tutaanza ku adapt hii teknolojia mpya. ikimaanisha kwamba hizi gari a mafuta tulizo nunua hivi karibuni kwa bei rahisi tutaachana nazo ili tununue gari mpya au tukaingia kugaramikia kubadili hizi gari za mafuta ziwe na teknolojia ya kisasa (ambapo kwa kweli itakuwa ni epensive sana)
Kwa hiyo tuamke sasa hii ni k**a WAKE UP CALL KWA WABUNIFU WA KIAFRIKA. ili tuweze kudhibiti tatizo hili kabla halija tuathiri sana.